... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kipofu Kuongoza Kipofu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 6:39,40 Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili? Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake.

Listen to the radio broadcast of

Kipofu Kuongoza Kipofu


Download audio file

Kuna hatari iliyo dhairi tena huwa iko daima kwa watu wanaoweka tumaini lao kwa mtu au kwenye kitu, wakiwemo Wakristo …..,ni kwamba wanaweza kutumia imani yao kutenda kitu cha ajabu hata kitu chenye hatari kabisa.

Ebu fikiria.  Ndivyo vita vibaya vile vya dini vilivyotokea kati ya mwaka 1095 na 1291, wakati Vita vya Msalaba vilitokea; au wakati uchunguzi wa Kanisa Katoliki uliweka mahakama ya kukomesha uasi kati ya karne ya 12 hadi katikati ya karne ya 15 – yalikuwa yale yale.  Au ukichukua wafia dini wanaojiripua siku hizi.

Kwa Mkisto, ukweli wa Injili ni ukweli unaovutia sana.  Na kuna walimu wengi katika Ukristo, walimu wenye nguvu, wanaohamasisha Wakristo kuinuka na kudai tena haki zao na kubadilisha taifa lao (po pote pale wanapoishi) liwe taifa la Kikristo.  Kweli hoja zao zina nguvu … walakini wamepoteza dira.

Luka 6:39,40  Akawaambia mithali, Je!  Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu?  Hawatatumbukia shimoni wote wawili?  Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake.

Usiruhusu viongozi vipofu wakupoteze.  Lengo la Injili, yaani Habari Njema ya Yesu Kristo, si kulazimisha mtu aikubali kwa lazima.  Kwa hiyo uwe na utambuzi.  Uwe makini kwa kuchagua waalimu wako.  Ni kweli, lazima tujishughulishe na utamaduni.  Tena lazima tusimame kidete kinyume cha uovu.  Lakini Injili ya Kristo ni Injili ya Upendo wa Mungu, msamaha wake, shauku lake la kuvuta watu kwake.

Usitumbukie shimoni.

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.