... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Wewe ni Jirani wa Namna Gani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kumbukumbu 22:1,2 Umwonapo ng’ombe wa nduguyo au kondoo wake akipotea, usijifiche kama usiyemwona; sharti utamrudisha kwa nduguyo. Na kwamba yule nduguyo hayupo karibu nawe, au ukiwa humjui, umchukue kwenu nyumbani kwako, uwe naye hata aje nduguyo kumtafuta, nawe mrudishie.

Majirani hua wana tabia ya kusumbuana.  Sababu inaweza kuwa mbwa anavyobweka, labda ni mizizi ya mti inayoranda chini ya fensi, labda ni moshi wa sigara au kufia mipaka.  Yaani kuwa jirani mwema ni changamoto sana!

Bila shaka sisi sote tumewahi kukosea katika changamoto za uhusiano na jirani.  Kulinda amani ni muhimu lakini Mungu anao wito wa hali ya juu kwetu kama majirani wa watu wengine.

Kumbukumbu 22:1,2  Umwonapo ng’ombe wa nduguyo au kondoo wake akipotea, usijifiche kama usiyemwona; sharti utamrudisha kwa nduguyo.  Na kwamba yule nduguyo hayupo karibu nawe, au ukiwa humjui, umchukue kwenu nyumbani kwako, uwe naye hata aje nduguyo kumtafuta, nawe mrudishie.

Ninataka kukuibia siri.  Majirani wangu nadhani hawana mifugo kama ng’ombe au kondoo, lakini juzi kampuni ya usafirishaji ilileta mzigo wa jirani yetu wakati hakuwa nyumbani.  Ilikuwa skrini mpya ya komputa ndani ya katoni na yule dereva aliiacha nje wakati wa mvua!  Wakati niliona inavyotaka kuloana, nilikubali kuloana mimi kwenda kuichukua isiharibike.  Jirani yetu alishukuru sana.  Sikugharimiwa lo lote lakini niliweza kumsaidia asipate hasara.

Ninataka kusema hivi.  Tumeagizwa kulinda na kujali majirani.  Si kulinda amani kati yetu tu, bali kujitolea na kukubali kusumbuka kwa ajili yao.  Kwa sababu matendo kama hayo ya kumsaidia mtu, ni ushuhuda tosha wenye nguvu wa upendo wa Mungu wetu ambaye tunakiri kwamba tunamwamini.

Umwonapo ng’ombe wa jirani au kondoo wake akipotea, usijifiche kama usiyemwona; sharti umrudishe kwa jirani yako.  

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.