... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Unasimama Wapi?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 19:25,26 Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, mama, tazama, mwanao.

Listen to the radio broadcast of

Unasimama Wapi?


Download audio file

Sijui kama umeshaona jinsi maisha yakiendelea shwari, unao watu wengi walio karibu yako, lakini wakati mambo yanaanza kukuharibikia, wengi wao wanatoweka?

Hii isingetushangaza.  Kwa sababu wakati mambo yanaanza kuwa magumu, ni kawaida mwanadamu kujaribu kukimbilia sehemu ya starehe na usalama.  Ni wachache mno wako tayari kukabiliana na matatizo yanayokukumba wewe.

Kwa hiyo swali inakuja:  Je!  Wewe ni mtu wa aina gani?  Uko tayari kusimama kidete licha ya magumu, au uko mtu atakayekimbia wakati wa matatizo?

Zamani, wakati Yesu alikuwa anatenda miujiza ya ajabu-ajabu, watu maelfu walimkusanyikia.  Yaani mji mzima uliweza kufunga kazi na kutoka kumkuta kwenye mbuga za malisho ili wamsikilize akifundisha.

Hatimaye alichagua watu kumi na wawili kati yao kukaa karibu naye.  Halafu kati ya hawa, ni watatu tu waliweza kumkaribia zaidi kwenye bustani ya Gethsemane kwa maombi usiku ule aliosalitiwa.  Halafu kesho yake, ilikuwa hivi:

Yohana 19:25,26  Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.  Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, mama, tazama, mwanao.

Msalabani pale, kulikuwa wanawake wanne (mmoja alikuwa mamaye) na mwanafunzi mmoja tu.  Sasa, wale wengine maelfu, au hata wale kumi na wawili walikuwa wapi?

Ukweli ndo huu:  Kadiri mtu anakaribia Msalaba, ndipo ataona kwamba watu wanazidi kupungua.  Kwa hiyo niulize, Je!  Wewe unasimama wapi?  

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy