... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Umtumikie Mungu kwa Moyo Mkamilifu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Mambo ya Nyakati 28:9 Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, nakuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

Listen to the radio broadcast of

Umtumikie Mungu kwa Moyo Mkamilifu


Download audio file

Je!  Umewahi kutendewa jambo fulani na mtu alilifanya kwa shingo upande?  Ni kama huwezi kulifuriahia vizuri kwa sababu hakulitenda na moyo wa upendo.

Lakini ukweli ni kwamba hata wewe na mimi, tunaweza kufanya kitu bila kupenda.  Tunaweza kukifanya kwa sababu ni wajibu tu, lakini moyoni tunanung’unika.  Siyo haki.  Kwa nini nimelazimika nilitende?

Zamani, wakati nilianza kusoma chuo cha Biblia, ilibidi tufanye kazi mbali mbali wakati hatuko darasani.  Kila mtu alipewa kazi fulani na hata kama nilikuwa nimeomba, “Tafadhali Bwana, nisipewe kazi ya kusafisha vyoo,” kumbe ndipo nilipowekwa kufanya usafi.

Wakati ule, nilikuwa bado ninafanya kazi katika kampuni ya teknolojia nikipanda ndege kwa daraja la fahari, nikichaji dola maelfu kwa siku kwa ajili ya ushauri wangu.  Sasa ni mimi nitafanya usafi ndani ya vyoo kwa kweli?  Unaona jinsi nilivyoweza kunung’unika.

Lakini Mungu alijua anachokifanya kwa sababu nilijifunza somo zuri sana.  Ni somo ile ile mzee Mfalme Daudi aliyomfundisha mwanae Sulemani:

1 Mambo ya Nyakati 28:9  Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, nakuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

Angalia sasa, kuna wakati Mungu anatuagiza tufanye mambo ambayo hatutaki.  Yafanye na moyo mweupe, moyo wa furaha kwa sababu anafahamu kinachoendelea moyoni.  Halafu ukimwendea kwa msaada, atakujibu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy