... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ujijenge Mwenyewe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu.

Listen to the radio broadcast of

Ujijenge Mwenyewe


Download audio file

Mwanariadha awaye wote atakwambia kwamba, ukitaka kupata nguvu zaidi, lazima ufanye mazoezi.  Shida ni kwamba, wengi wetu, na mimi nikiwemwo, hatupendezwi na kufanya mazoezi.

Wakati alikuwa na umri wa miaka 15, mchezaji wa filamu huko Hollywood, aitwaye Arnold Schwarzenegger aliamua kwamba alitaka kuwa wa kwanza kabisa duniani kote kuwa na nguvu kuliko wanaume wengine – kwa hiyo alianza kufanya mazoezi ya kujenga mwili wake – akayafanya masaa matano hadi sita kwa siku.

Mimi simo kabisa.  Ninafanya mazoezi kidogo, lakini yeye alizidi kabisa kwa maoni yangu.  Kinachohuzunisha sana ni kwamba mtazamo kama huo, ndio watu wengi wanao kuhusu maombi.

Subiri kwanza … tumehamiaje kutoka mada ya mazoezi ya kujenga mwili na kuanza kuongea habari ya maombi?  Ni kwa sababu imeandikwa hivi:

Yuda 1:20  Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu.

Kwa hiyo, mtu anazidi kupata nguvu kwa kupitia maombi akisaidiwa na Roho Mtakatifu.  Lakini hata hivi, watu wa Mungu wengi hawachukui muda mzuri kila siku katika maombi yasiyo na haraka.

Swali:  Je!  Unataka kuwa mdhaifu au mwenye nguvu katika imani yako?  Je!  Unataka kupelekwa huku na huko na mawimbi ya bahari au uko tayari ndani ya Kristo kusimama kidete licha ya changamoto za maisha?

Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy