... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Si wa Kwetu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 9:38-41 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninena mabaya; kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu. Kwa kuwa atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amini, nawaambia, hatakosa thawabu yake.

Listen to the radio broadcast of

Si wa Kwetu

Download audio file

Ninaendelea kushangaa mno nikiangalia jinsi tumetawaliwa na ukabila na vikundi siku hizi, bila hata kufahamu.  Hua inatokea kwenye michezo, na kwenye siasa pia, na hii haishangazi sana.  Lakini ukabila unaonekana pia kwa chini chini na kwa njia mbali mbali.

Penda, usipende, jamii inaweka vikundi vikundi kufuatana na uwezo wa kipato.  Ina maana, matajari hua wanapenda kukaa na matajiri wengine; wao wa kati na wa kati wenzao, maskini na maskini wenzao.  Ni kweli, kuna wengine hawajali mgawanyiko huo, lakini ni wachache.  Ndivyo ilivyo.

Isitoshe, tunao asili au mwelekeo kujitenga na watu ambao hatufanani, watu ambao wana lugha tofauti, wenye maono na imani tofauti.  Nina uhakika kama tungejichunguza kidogo, tungeweza kugundua ubaguzi fulani maishani mwetu.

Mariko 9:38-41  Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi.  Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninena mabaya; kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.  Kwa kuwa atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amini, nawaambia, hatakosa thawabu yake.

Usiwe haraka kwa kuhukumu mtu mwingine.  Usiwe haraka kujenga ukuta.  Yesu alikufa kwa ajili ya sisi sote.

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy