... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Pale Moyo Uliovunjika Unabadilishwa na Kuwa Baraka

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yeremia 17:14 Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.

Listen to the radio broadcast of

Pale Moyo Uliovunjika Unabadilishwa na Kuwa Baraka


Download audio file

Labda nitakusumbua kwa maswali leo!,  Hivi, Umewahi kuvunjika moyo?  Je!  Umewahi kuhisi kama mambo yako hayako sawa!?; ya kwamba hauna nguvu tena za kupambana na yale yote unayokabiliana nayo!?

Huwa hatupendi kueleza hali hiyo mara kwa mara … lakini zaidi na zaidi, simu yangu inapokea njumbe mbalimbali zikiuliza ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuboresha afya yake au kuongeza nguvu za kufanya kazi pindi tu anapoamka asubuhi, au namna ambavyo watu wengine huwa hawasemi ukweli  pale wanapokwenda kwa mtaalamu wa maswala ya akili ili kupata ushauri wa kisaikolojia.

Kuna mambo mengi huwa yanatuchanganya, unakuta tunaishi maisha yasiyoridhisha  na kwa njia moja ama nyigine, sote kuna wakati huwa tunavunjikamoyo.

Lakini, hata wataalamu  huwa wanapapasa papasa tu, Ni kweli, kuna mambo ya msingi mtu anapaswa afanye – kula vizuri, kufanya mazoezi, upate usingizi wa kutosha, mtu awe  na mahusiano mazuri na watu wengine.  Hayo yote yanafaa sana.

Lakini mwisho wa siku, kuna njia moja ya kubadilisha hali ya moyo uliopondeka na kuwa baraka.

Yeremia 17:14  Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.

Mungu pekee ndiye awezaye kukutibu kikwelikweli, YEYE ndiye awezaye kukujaza na utukufu wake, kukuzidishia pendo lake, kukutibu kwa njia ya Roho wake na kukupa yote unayohitaji, si kukunusuru tu usife!, bali  hata kukustawisha vizuri hata kama maisha yanakuwia vigumu kiasi gani.

Kwasababu akikuponya, hakika utaponyeka.  Akikuokoa, hakika utaokoka. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy