... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu Alikuumba kwa Ajili ya Ushindi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 15:56-58 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.

Listen to the radio broadcast of

Mungu Alikuumba kwa Ajili ya Ushindi


Download audio file

Dhana ya kuishi maisha ya ushindi inavutia; lakini pia inaweza kuelezwa vibaya hususani katika ulimwengu wetu wa kisasa wa wanadamu wanaofikiri kwamba mafanikio ndiyo lengo na madhumuni ya kuwepo duniani.  Ni rahisi kufikiri kwamba ushindi ni kushinda kila kitu: Mungu naye ana mtazamo tofauti kabisa kuhusu maisha ya ushindi.

Kwa mtazamo wa Mungu, kuishi maisha ya ushindi ni kushinda uchungu wa mauti unaotokana na matendo yetu maovu, yaani dhambi zetu hapa duniani na kuendela milele na milele.

Sawa, lakini kwa mtazamo wa haraka haraka, haivutii sana, namna tunayovutwa na mafanikio katika shughuli zetu na dhidi za mazingira yetu na changamoto zote za maisha kwa kufuta kabisa matatizo yote.  Sijui kama tuko pamoja?

Kwahiyo ninakusihi, jaribu kuangalia swala hili la ushindi kwa mtazamo wa Mungu, tafadhali:

1 Wakorintho 15:56,57  Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.  Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.    

Kwa hiyo, ushindi ni karama itokayo kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.  Tukiwa na mahusiano mazima yanayosisimua na kutembea kwa kutii amri za Mungu, wewe na mimi tutapewa ushindi dhidi ya dhambi zetu.  Si kwamba hatutapata matatizo maishani!? (Yesu aliwaahidia wanafunzi wake na sisi pia kwamba ulimwenguni tutapata dhiki!) lakini tunaweza kushinda uchungu wa mauti unaoletwa na dhambi zetu – katika maisha haya na maisha ya baadaye.  Hii ni bora kuliko mafanikio. 

Rafiki yangu, Mungu alikuumba ili uishi maisha ya ushindi sasa hivi hadi milele yote.

Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.      

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy