... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Msingi wa Wokovu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Matendo 16:29-31 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

Listen to the radio broadcast of

Msingi wa Wokovu


Download audio file

Ni vizuri mara kwa mara kujikumbusha mambo ya msingi,  Halafu jambo muhimu na la msingi kuliko yote; ni kujua mahali mtu utaishi milele, eee, kwasababu milele ni muda mrefu sana tena usio na mwisho.

Sasa, hili ni jambo ambalo Mungu ameweka wazi kabisa, kwamba mtu akifa, nafsi yake inaendelea kuishi milele – ama mbele za Mungu, au kwenye mateso huko Jehanamu.

Yaani, ni mada yenye nguvu inayozungumzwa mara nyingi ndani ya Biblia, tena haiwezi kugushiwa kwa kusema, “Najua mimi si mkamilifu lakini kwa kuwa Mungu ananipenda nitakuwa sawa tu”, hapana.  Je!  Unataka kubahatisha umilele wako ukiwa na mashaka-mashaka?

Je!, Mtu anawezaje kuhakikisha kwamba anaelekea pazuri?  Swali hili lilimsumbua mtu fulani aliyetoka kushuhudia muujiza mkubwa:

Matendo 16:29-31  Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?  Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

Njia pekee ya kuokolewa na adhabu ya milele ndani ya Jehanamu ni kumwamini Yesu. Lakini ni kumwamini kwa kutegemeza maisha yako yote mikononi mwake – kila sehemu.  Kwa hiyo …

Yakupasa ufanye nini upate kuokoka?  Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy