Jihadhari!
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Mathayo 6:1,2 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
Kuona mtu anajitanguliza na kujipendekeza daima haipendezi hata kidogo. Watu kusema au kutenda hadharani ili watu wawasifu inachukiza. Kwa nini wanafanya hivi?
Juzi, niliona picha ya “selfie” mtu alijipiga kwenye Instagram akitoa chakula kwa maskini katika nchi ambayo haijaendelea sana. Nilishangaa mno. Watu wanataka kujitukuza kwa njia ya kitendo cha ujinga hicho?
Lakini mtu akichunguza vizuri atagundua ukweli huu: Sisi sote tunapenda kutukuzwa. Ndivyo tulivyo. Halafu katika ulimwengu huu wa kisasa tunamoishi, kila mtu akiwa na simu janja mkononi, nikiangalia jinsi watu wanajitukuza na kujitangaza mtandaoni, naona kwamba dunia imefikia sehemu ya ajabu sana!
Na hata kama mtu hatafuti kujulikana kwa kiburi, ukipitia yale aliyoyaweka mtandaoni katika tovuti zake za kijamii, utaona picha zinazoeleza ubora wa maisha yake tu.
Sio rahisi kutenganisha nia ya kawaida ya mtu kujionyesha kwamba ni mtu anayefaa na nia ya mtu kujitukuza sana. Yaani siku hizi ni vigumu mno kujua ni wapi mtu ameangukia. Ndiyo maana Yesu aliweka tahadhari hii …
Mathayo 6:1,2 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.