... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Chumvi Isiyo na Ladha Tena

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 9:50 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, makakae kwa amani ninyi kwa ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Chumvi Isiyo na Ladha Tena


Download audio file

Chumvi ni kitu ambacho tunatumia kila siku kwa kukoleza chakula chetu kwa kuboresha ladha yake.  Lakini hata kama chumvi ni muhimu sana kwa binadamu, mara nyingi hatuwazi sana juu yake.

Katika enzi za kale, chumvi ilikuwa na thamani kubwa kuliko hata dhahabu.  Siku hizi bei yake ni chini sana.  Lakini kama mtu angebadilisha chumvi yako akaweka unga usio na ladha, ungefanyaje?  Si ungeitupa nje? Na lengo la Yesu alitaka kusema hivi:

Mariko 9:50  Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee?  Mwe na chumvi ndani yenu, makakae kwa amani ninyi kwa ninyi.

Anatoa mfano kwa kulinganisha utamu na faida ya chumvi na maisha ya mmoja wao wa wanafunzi wake.  Anayemwamini Yesu awaye wote akimwishia yeye, anaye Roho wake, Roho Mtakatifu hukaa ndani yake.

Hii inatupa nafasi pana kukoleza maisha ya watu wengine, ni fursa ya kipekee kuonyesha upendo wa kujitolea, wema, upole,hekima na unyenyekevu – vyote vikiongeza utamu ndani ya maisha yao kwa jinsi isiyoweza kuelezeka.

Lakini kama hatumruhusu Yesu kutubadilisha na kuwa mtu kama yule ambaye tumetoka kumtaja, basi imani yetu kwake na hata Roho yake ndani yetu haina kazi tena, vitakuwa kama unga tu mweupe usio na ladha yo yote.

Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee?  Mwe na chumvi ndani yenu, makakae kwa amani ninyi kwa ninyi. 

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy